• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China akutana na waziri mkuu wa Hispania

    (GMT+08:00) 2018-11-29 07:04:14

    Rais Xi Jinping wa China ambaye yuko ziarani nchini Hispania, amefanya mazungumzo na waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Pedro Sanchez.

    Pande hizo mbili zimefikia maafikiano kuhusu kuhimiza uhusiano kati ya nchi zao, na kuchukulia maadhimisho ya miaka 45 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kuwa mwanzo mpya.

    Wakati wa mazungumzo hayo, rais Xi amesisitiza kuwa China inaunga mkono mafungamano ya Ulaya. China na Ulaya zinatakiwa kuimarisha ushirikiano katika kulinda kwa pamoja utaratibu wa kimataifa na kuhimiza usimamizi wa mambo ya dunia. Pia ameeleza kuwa China inapenda kuimarisha juhudi za kuoanisha Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na mikakati ya maendeleo ya Umoja wa Ulaya, ili kuhimiza kwa pamoja mawasiliano kati ya Asia na Ulaya, na ustawi wa mabara hayo mawili.

    Naye Bw. Sanchez amesisitiza kuwa Hispania inaunga mkono kithabiti utaratibu wa pande nyingi, na inapenda kuimarisha mawasiliano na China, ili kuhimiza uhusiano kati yao kupata maendeleo kwa hatua madhubuti.

    Viongozi hao wawili pia wamekutana kwa pamoja na wajumbe wa pande hizo mbili katika Kamati ya washauri wa viwanda vya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako