• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Usajili dirisha dogo unaendelea, Stand United yatambulisha kifaa kipya, mrithi wa Kapombe atua Msimbazi

    (GMT+08:00) 2018-11-29 08:43:40

    Siku chache baada ya shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) kutangaza kufungua dirisha dogo la usajili, klabu mbalimbali zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara zinaendelea na zoezi la usajili.

    Klabu ya Stand United (Chama la Wana) imewatema wachezaji wake wanne huku ikifanikiwa kunasa saini ya mchezaji mmoja pekee hadi sasa.

    Nao mabingwa watetezi wa ligi hiyo Simba ya Dar es salaam imemshusha beki wa kulia Zana Coulibaly kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast kuziba pengo la beki wake Shomari Kapombe ambaye anaendelea na matibabu nchini Afrika Kusini baada ya kuumia wakati akiichezea timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars dhidi ya Lesotho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako