• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanahabari wa Rwanda anayefanya kazi BBC akamatwa kwa tuhuma za ugaidi

    (GMT+08:00) 2018-11-29 08:43:51

    Shirika la upelelezi la Rwanda RIB limesema mwanahabari mmoja wa Rwanda anayefanya kazi na Shirika la utangazaji la Uingereza BBC amekamatwa kwa tuhuma za ugaidi. Msemaji wa RIB Bw. Modeste Mbabazi amesema mjini Kigali kuwa Bw. Phocas Ndayizera alikamatwa Jumatano iliyopita kwenye eneo la Nyamirambo, pembezoni mwa mji mkuu Kigali, ambako alikuwa ameenda kupokea "milipuko".

    Bw. Mbabazi amesema mwanahabari huyo alikamatwa na mtu mwengine aliyempatia milipuko. Bw. Ndayizera ambaye anafanya kazi na Idhaa ya Kinyarwanda ya BBC, amekataa tuhuma hizo na kusema hajui atakabiliwa na mashtaka gani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako