• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watengenezaji bidhaa wa Rwanda wahimizwa kuhakikisha ubora wa bidhaa zao

    (GMT+08:00) 2018-11-29 08:44:08

    Waziri wa biashara wa Rwanda amewahimiza watengenezaji wa bidhaa wa Rwanda kuhakikisha ubora wa bidhaa zao ili kuendeleza kampeni ya kuhimiza "Made-in-Rwanda", wakati maonesho ya bidhaa zinazotengenezwa na Rwanda yanafanyika.

    Maonesho ya nne ya "Made in Rwanda" yanayofanyika kuanzia Novemba 28 hadi Desemba 4 mjini Kigali, yamevutia waonesha bidhaa 450 kutoka sekta mbalimbali, zikiwemo TEHAMA, kilimo, nguo, ujenzi na uzalishaji viwandani.

    Akiongea kwenye maonesho hayo, waziri wa biashara na viwanda wa Rwanda Bibi Soraya Hakuziyaremye ametoa mwito kwa wanyarwanda kutumia zaidi bidhaa zilizotengenezwa Rwanda. Pia amewataka watengenezaji wa bidhaa kuhakikisha wanaongeza thamani ya bidhaa zao na kuzalisha bidhaa zenye ubora, ambazo zinaweza kushindana kwenye masoko ya ndani na kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako