• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU watafakari utekelezaji kwa mafanikio wa mpango wa mpito nchini Somalia

    (GMT+08:00) 2018-11-29 08:44:27

    Ujumbe kutoka Kitengo cha Msaada wa Amani (PSD) cha Umoja wa Afrika umemaliza ziara ya siku tatu nchini Somalia, ukitoa wito wa kufanikisha utekelezaji wa mpango wa mpito katika mfumo wa usalama nchini humo.

    Ujumbe huo wenye wajumbe 27 unaoongozwa na balozi wa Djibouti nchini Ethiopia Bw. Mohamed Idriss, pia umeahidi kutathmini kwa makini hali ya nchi hiyo.

    Bw. Idriss amesema wanatumai mkutano wa viongozi wa kijeshi kutoka nchi sita zilizotuma vikosi nchini Somalia unaotarajiwa kufanyika kesho, utapitisha mkakati mpya wa kuondoka kwa vikosi vya Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM, ambao unalenga kutoa mwongozo kwa operesheni za AMISOM kuanzia mwaka huu hadi mwaka 2021, ikiwa ni kipindi cha mwisho cha mpito wa tume hiyo kabla ya kuondoka kabisa nchini Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako