• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Matokeo ya ligi ya mabingwa ulaya hatua ya makundi

    (GMT+08:00) 2018-11-29 08:46:44

    Ligi ya mabingwa barani ulaya imeendelea usiku wa jana na kutoa matokeo magumu kwa baadhi ya timu na baadhi kukata tiketi za hatua ya 16 bora na kuna ambao wataenda kujiuliza katika ligi ya washindi barani Ulaya maarufu kama UEFA champions league na baadhi zitayaaga kabisa mashindano hayo na kusubiri msimu ujao wa 2019/20.

    Kundi A, Atletico Madrid imeibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Monaco, huku Borussia Dortmund ikilazimishwa sare ya 0-0 na Club Brugge, kundi B, PSV Eindhoven imekubali kipigo cha 1-0 toka kwa Barcelona, nayo Tottenham Hotspur ikiikalisha Inter Milan kwa goli 1-0. Mchezo ulioteka mashabiki wengi ulikuwa wa kundi C kati ya Paris Saint Germain (PSG) na Liverpool, PSG imechomoza na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Liverpool, nayo Napoli ikiichakaza FK Crvena Zvezda kwa magoli 3-1, na mechi za mwisho ni za kundi D, Lokomotiv Moscow ikiifunga Galatasaray kwa jumla ya magoli 2-0 na FC Porto ikiinyeshea mvua ya magoli 3-1 Schalke 04.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako