• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia yataka kuimarisha sheria ya kupambana na ukatili wa kijinsia

    (GMT+08:00) 2018-11-29 08:56:40

    Serikali ya Zambia imesema itaimarisha shera zake zinazohusu ukatili wa kijinsia, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha inapambana na tatizo hilo.

    Waziri wa jinsia wa Zambia Bibi Elizabeth Phiri amesema licha ya hatua mbalimbali zilizochukuliwa, Zambia bado haijapiga hatua kwenye kupambana na tatizo hilo, na badala yake linaonekana kuongezeka.

    Amesema wanawake wanafuta kesi wanapokumbwa na matumizi ya mabavu nyumbani, kwa kuwa wanawategemea wanaume kifedha, na hawataki kuona wanaume hao wanaoleta chakula kwenye familia wakipelekwa gerezani.

    Mbali na Zambia, Msumbiji nayo imejiunga na kampeni ya umoja wa mataifa yenye lengo la kuhimiza usawa wa kijinsia duniani. Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji amesema, kwa kuwashirikisha wanaume na wavulana kwenye kampeni hiyo, kutafanya kuwe na kizazi cha watu wanaotambua changamoto zilizopo, na wakati huo huo kuwa washiriki muhimu kwenye mapambano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako