• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yazitaka nchi za Afrika Mashariki kutumia mfumo wa manunuzi ya umma kwa mtandao ili kupambana na ufisadi

    (GMT+08:00) 2018-11-29 08:57:00

    Kenya imezitaka nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki kutumia mfumo wa Tehama kwenye manunuzi ya serikali, ili kupambana na ufisadi. Waziri wa fedha wa Kenya Bw. Henry Rotich amesema kwenye kongamano la mambo ya fedha mjini Nairobi, kuwa ufisadi unatakiwa kuondolewa ili kurudisha imani ya umma na ushindani wa haki.

    Bw. Rotich amesema manunuzi ya umma ni shughuli kubwa ya kiuchumi inayoingiza fedha nyingi kwenye uchumi wa nchi. Hali hiyo inafanya manunuzi hayo kuwa moja ya maeneo yenye hatari kubwa ya kukumbwa na ufisadi.

    Kwenye kongamano lingine lililofanyika mjini Kigali, kuwakutanisha maofisa wa nchi za Afrika wanaopambana na ufisadi, mwendesha mashtaka wa serikali ya Afrika Kusini Bw. Busisiwe Mkhwebane, amesema kutokuwa na fedha za kutosha kunafanya uchunguzi wa malalamiko ya wananchi kuhusu ufisadi uwe mgumu.

    Mjini Dar es salaam aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Bw. Thabo Mbeki amekutana na Rais John Magufuli wa Tanzania na kufahamishwa juhudi za Tanzania katika kupambana na utakatishaji fedha, ufisadi na utoroshaji wa fedha katika sekta ya madini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako