• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo kati ya Uganda na DRC kuhusu operesheni ya pamoja dhidi ya waasi wa ADF yaahirishwa

    (GMT+08:00) 2018-11-29 09:21:34

    Msemaji wa jeshi la Uganda Brigedia Jenerali Richard Karemire amesema, mazungumzo kati ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC kuhusu operesheni ya pamoja dhidi ya kundi la uasi la ADF yaliyopangwa kufanyika wikiendi hii, yameahirishwa ili kutoa nafasi ya majadiliano zaidi.

    Msemaji huyo amesema, mazungumzo hayo kuhusu operesheni ya pamoja dhidi ya waasi wa ADF ambao hivi karibuni waliwaua walinzi wa amani na askari wa DRC, bado yanapangwa. Tarehe nyingine ya kufanyika kwa mazungumzo hayo itatangazwa baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako