• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanadiplomasia nchini China watembelea wilaya ya Dali, mkoani Shaanxi

    (GMT+08:00) 2018-11-29 18:42:23

    Wanadiplomasia katika kijiji cha Yantong wilayani Dali

    Katika miaka ya hivi karibuni, wilaya ya Dali mkoani Shaanxi, China imeendeleza kilimo kwa nguvu kubwa, huku maisha ya wakulima yakiboreshwa kwa kiasi kikubwa.

    Tarehe 30 mwezi Oktoba, wanadiplomasia wa nchi mbalimbali nchini China wakiwemo mabalozi na wanadiplomasia wengine wa Afrika Kusini, Iran, Tanzania, Rwanda, Somalia na Mauritius walitembelea vijana kadhaa vya wilaya hiyo, ili kuhimiza ushirikiano, na kuisaidia wilaya ya Dali kujulikana duniani.

    Katika kijiji cha Yantong, wanadiplomasia hao walivutia macho ya watu wengi huko, na walisalimiana na kupiga picha kwa pamoja. Wanadiplomasia hao pia walitembelea nyumba za wakulima, na kushuhudia maisha yao.

    Balozi wa Afrika Kusini nchini China Debora Balatseng

    Balozi wa Afrika Kusini nchini China Bi. Debora Balatseng alipohojiwa na waandishi wa habari wa mkoa wa Shaanxi alisema, anaona watu wa wilaya ya Dali wanaishi maisha bora, wana nyumba nzuri na vifaa vyote vinayohitajika maishani. Mwanadiplomasia wa Tanzania Bw. Joseph Laizer alisema anawapenda watu hao, kwani ni wakarimu, wanajiamini, na wana afya na furaha.

    Kijiji cha Pingluo kiko karibu na kijiji cha Yantong. Mwaka 2017, wastani wa kipato cha mwanakijiji ulifikia yuan 13, 650 sawa na dola za kimarekani karibu 2,000. Kijiji hicho ni kijiji cha kisasa cha kielelezo mkoani Shaanxi.

    Wanadiplomasia wanatembelea kibanda cha maua kijijini Luoping

    Baada ya kutembelea kibanda cha maua na kujaribu matunda ya kijiji cha Luoping, balozi mdogo wa Somalia nchini China Bw. Ali Mohamed Hussein aliuliza kama kuna uwezekano wa kufanya ushirikiano. Mkuu wa kijiji hicho alijibu, ndiyo!

       Balozi mdogo wa Somalia nchini China Bw. Ali Mohamed Hussein anahojiwa na waandishi wa habari wa mkoa wa Shaanxi

    Bw. Ali alisema Somalia ni nchi kubwa ya kilimo, idadi kubwa ya watu ni wakulima, na kuna aina nyingi za matunda nchini humo. Lakini kutokana na hali duni ya teknolojia, kipato cha wakulima ni kidogo. Alisema anatumai kujifunza teknolojia za kisasa za kilimo za China, ili kuisaidia nchi yake kuendeleza uchumi.

    Mwanadiplomasia wa Tanzania Bw. Joseph Laizer anapiga picha na wanakijiji wa Yantong

    Mkurugenzi wa idara ya ushirikiano wa teknolojia ya wilaya ya Dali Bi. Zhang Huanling amesema, anatarajia kufanya ushirikiano na nchi za Afrika, na huu utakuwa utekelezaji wa moyo wa mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Beijing.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako