• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yatarajiwa kusaidia kuangamiza magaidi jimboni Idlib

    (GMT+08:00) 2018-11-29 18:51:14

    Mjumbe wa rais wa Russia anayeshughulikia suala la Syria Bw. Alexander Lavrentyev amesema, operesheni ya kuliangamiza kundi la Nusra Front na makundi mengine ya kigaidi itaendelea kufanyika hadi makundi yote yatakapotokomezwa.

    Bw. Lavrentyev amesema hayo kwenye mkutano wa siku mbili wa suala la Syria uliofanyika mjini Astana, Kazakhstan. Amesema, hivi sasa, wapiganaji elfu 15 bado wako kwenye jimbo la Idlib, na Russia inapenda kushirikiana na jeshi la serikali la Syria kuwaondoa.

    Akizungumza kuhusu suala la kuunda kamati ya katiba, Bw. Lavrentyev amesema, Russia, Iran na Uturuki zitamsaidia kadri ziwezavyo mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika suala hilo Bw. Steffan de Mistura kutoa orodha ya kamati hiyo ambayo itaridhisha pande zote za Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako