• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza yaweza kupoteza alama 8 za ukuaji wa GDP kama ikiondoka bila mpangilio kwenye Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2018-11-29 18:53:57

    Benki Kuu ya Uingereza imesema kama nchi hiyo itaondoka bila mpangilio mzuri kwenye Umoja wa Ulaya inaweza kupoteza asilimia 8 ya ukuaji wa pato la taifa (GDP) katika miaka mitano ijayo.

    Ripoti iliyotolewa jana na Benki hiyo imesema, upotevu wa asilimia 8 katika ukuaji wa GDP kati ya mwezi Novemba mwaka huu na mwisho wa mwaka 2023 unaweza kutokea katika kile ilichogundua kuwa ni athari mbaya ya Brexit wakati mchakato wa kutoka utamalizika rasmi lakini bila ya makubaliano yoyote kuhusu biashara na ushuru.

    Pia Benki hiyo imesema, kutoka bila mpangilio kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya pia kunamaanisha kuwa nchi hiyo itafanya biashara na Umoja wa Ulaya chini ya kanuni za Shirika la Biashara Duniani (WTO), hivyo kuongeza vizuizi na gharama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako