• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatarajia ziara ya rais wa Ujerumani kuongeza uaminifu wa kisiasa na kimkakati kati ya nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2018-11-29 19:05:04

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo hapa Beijing amesema, rais Frank-Walter Steinmeier wa Ujerumani atafanya ziara nchini China kuanzia tarehe 5 hadi tarehe 10 mwezi ujao, ikiwa ni ziara yake ya kwanza nchini China tangu ateuliwa.

    Bw. Geng Shuang amesema, uhusiano kati ya China na Ujerumani umeendelezwa vizuri mwaka huu, ushirikiano katika sekta za uchumi, biashara na uwekezaji umepata matokeo mapya, na thamani ya biashara kati ya nchi hizo mbili imefikia kiwango cha juu zaidi kihistoria. Wakati huo huo, China na Ujerumani zimefanya uratibu na ushirikiano mzuri katika kulinda kwa pamoja utaratibu wa pande nyingi na biashara huria, kuhimiza uchumi wazi wa dunia, na kusukuma mbele maendeleo ya amani na utulivu wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako