• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wakana kuuawa kwa askari wake katika shambulizi lililofanywa na kundi la Al Shabaab kusini mwa Somalia

    (GMT+08:00) 2018-11-29 19:06:03

    Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika kimekana madai kuwa baadhi ya askari wake wameuawa na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab katika jimbo la Lower Shabelle, kusini mwa Somalia.

    Taarifa iliyotolewa na Kikosi hicho imefafanua kuwa, askari wake waliokuwa wanafanya doria walizuia kwa mafanikio shambulizi lililofanywa na wapiganaji hao huko Gandawi. Taarifa hiyo imesema hakuna vifo wala majeruhi kama ambavyo ripoti zinadai, na kwamba madai hayo ni propaganda ya kundi la Al Shabaab.

    Taarifa hiyo pia imesema kikosi hicho ambacho kimeongeza mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa kundi hilo, hakitasita kuendelea na majukumu yake, na kufanya kazi kwa pamoja na vikosi vya usalama vya Somalia ili kuhakikisha usama wa nchi na kuwalinda wananchi wanaopenda amani wa Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako