• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Waziri wa biashara na viwanda wa Rwanda atoa wito wa kuboreshwa kwa bidhaa

    (GMT+08:00) 2018-11-29 19:29:52
    Waziri wa biashara na viwanda wa Rwanda, Soraya Hakuziyaremye, amesema juhudi zaidi zinahitajika kutoka kwa serikali na sekta ya kibinafsi ili kuongeza ubora na wingi wa bidhaa zinazotengenezewa nchini humo.

    Akizungumza mbele ya kufunguliwa kwa maonyesho ya bidhaa za Rwanda, waziri huyo amesema mauzo ya nje ya nchi hiyo yameongezeka kwa asilimia 70 tangu kuanzishwa jwa sera ya kutengeneza bidhaa ndani ya nchi na kuleta dola milioni 944.

    Alisema wazalishaji bidhaa wanafaa kuzingatia ubora unaotosheleza mahitaji ya soko la nyumbani na pia kuongeza uzalishaji wao ili kujinufaisha na soko la kimataifa.

    Waziri Soraya amesema pia serikali inatafuta njia za kupata maligafi kutoka nchi za karibu kama vile ngozi kutoka Ethiopia badala ya kununua kwenye masoko ya mbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako