• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Mradi mpya wa ndizi waanzishwa kwenye wilaya tano Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-11-29 19:30:09
    Mradi mpya wa kilimo nchini Rwanda unatarajiwa kuongeza uzalishaji wa ndizi kwenye wilaya tano.

    Mradi huo uliozinduliwa leo unalenga wilaya za Gisagara, Muhanga, Karongi, Rwamagana and Rubavu.

    Utaendeshwa kwa miaka miwili na utajumuisha upanzi wa miche 60,000 za aina mpya ya migomba.

    Mradio huo unatekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya Rwanda na shirika la chakula na kilimo duniani FAO.

    Mwakilishi wa FAO nchini Rwanda Gualbert Gbehounou amesema wangependa wakulima wawe washindane ili kufanikisha lengo la kujitosheleza na ndizi.

    Kwa jumla nchini Rwanda ndizi huchukua asilimia 23% ya eneo lote la kilimo ambalo ni ekari 900,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako