• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi ya Mabingwa barani Afrika: Simba na Gor Mahia zaanza vizuri

  (GMT+08:00) 2018-11-29 19:37:59

  Klabu ya Simba ya Dar es salaama Tanzania imeanza vyema michuano ya ligi ya mabingwa Afrika baada ya kuirarua Mbabane Swallows ya Eswatini zamani Swaziland magoli 4-1 katika mchezo wa raundi ya awali ya ligi hiyo uliochezwa jana uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

  Ushindi huo unamaanisha Simba SC imerahisisha kazi kuelekea mchezo wa marudiano Desemba 4 nchini Swaziland, kwani wenyejii watatakiwa kushinda 3-0 ili kusonga mbele.

  Timu nyingine iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Afrika Mashariki na Kenya katika michuano hiyo ni Gor Mahia ilipoifunga kwa taabu Nyasa Big Bullets kutoka Malawi kwa goli 1-0 kwenye uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako