• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Katibu mkuu akagua maendeleo ya maboresho ya uwanja wa Taifa kwa ajili ya mashindano ya AFCON U17

    (GMT+08:00) 2018-11-30 08:33:25
    SOKA: Katibu mkuu akagua maendeleo ya maboresho ya uwanja wa Taifa kwa ajili ya mashindano ya AFCON U17

    Katibu mkuu wizara ya habari, utamaduni, Sanaa na michezo wa Tanzania Bi. Susan Mlawi amemtaka mkandarasi anayefanya ukarabati wa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kuhakikisha anamaliza kazi kwa wakati kuelekea mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 yanayotarajiwa kufanyika nchini Tanzania mwanzoni mwa mwakani.

    Bi. Susan amesema hayo alipotembelea uwanja huo kukagua ukarabati unaoendelea chini ya usimamizi wa kampuni ya uhandisi na ujenzi ya Beijing toka China.

    Mkandarasi toka kampuni hiyo bwana Zhang Jiawa amemuhakikishia katibu mkuu huyo kuwa kazi hiyo itakamilika kwa wakati na kuahidi kukabidhi kazi hiyo mapema mwanzoni mwa mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako