• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi kuu Tanzania Bara (TPL) Yanga yaishusha Azam kileleni

  (GMT+08:00) 2018-11-30 08:34:18

  Mabingwa mara 27 wa ligi kuu Tanzania bara Yanga, jana imepanda kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuichapa JKT Tanzania kwa mabao 3-0 mchezo uliochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

  Mabao ya Yanga yamefungwa na Herities Makambo, Mrisho Ngasa na bao la penalti limefungwa na Ibrahim Ajib yalitosha kuwafanya mashabiki wa Yanga kusahau shida na matatizo ya ukata yanayoikabili klabu hiyo kwa sasa.

  Ushindi huo umepelekea Yanga kuongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 35 baada ya kucheza mechi 13, ikifuatiwa na Azam fc yenye pointi 33 huku Simba SC ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi 27.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako