• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Issa Hayatou na Hicham El Amrani wajibu baada ya kuhukumiwa

    (GMT+08:00) 2018-11-30 08:35:37

    Rais wa zamani wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Issa Hayatou na aliyekuwa katibu mkuu Hicham El Amrani wametozwa faini ya dola milioni 27.9 kila mmoja na mahakama ya uchumi nchini Misri (EEC).

    Mahakama hiyo imesema kuwa wawili hao walivunja sheria ya nchi hiyo kwa kutia saini mkataba wa dola bilioni moja kati ya CAF na kampuni ya Ufaransa ya Lagardere mwaka 2015.

    Sheria ya Misri, inaeleza, kupata mkataba huo, lazima uwe wazi kwa kila mmoja lakini haikuwa hivyo. Hata hivyo, El Amrani na Hayatou wamesema watakata rufaa kuhusu faini hiyo. Aidha, wanasema kesi hiyo imechochewa kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako