• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa Rwanda wakua kwa asilimia 8.9 katika mwaka wa fedha 2017/18

    (GMT+08:00) 2018-11-30 08:58:34

    Benki kuu ya Rwanda imesema uchumi wa Rwanda umekua kwa asilimia 8.9 katika mwaka wa fedha 2017/18, ikilinganishwa na asilimia 3.4 ya mwaka uliotangulia.

    Akiwasilisha ripoti ya benki kuu kwenye kikao cha bunge mjini Kigali, Gavana wa benki kuu ya Rwanda Bw. John Rwangombwa amesema ukuaji huo wa uchumi unatokana na hali nzuri ya hewa kwa uzalishaji wa kilimo, kufufuka kwa sekta ya ujenzi na kuboreka kwa bei za bidhaa za kimataifa.

    Bw. Rwangombwa amesema utendaji mzuri wa uchumi wa dunia pia ulichangia ongezeko la asilimia 57.6 la uuzaji nje wa bidhaa za Rwanda kwa mwaka huu, ikilinganishwa na asilimia 7.1 ya mwaka jana, ukuaji ambao ulipunguza urari mbaya wa Rwanda kwenye biashara za kimataifa kwa asilimia 21.1.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako