• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vijana wa Sudan Kusini washiriki kwenye mazungumzo ili kutokomeza matatizo ya kijamii

    (GMT+08:00) 2018-11-30 08:58:53

    Vijana wa Sudan kusini kutoka jimbo la Jonglei, lililoko mashariki mwa nchi hiyo, wameshiriki kwenye mazungumzo ili kutokomeza matatizo ya kijamii ikiwemo wizi wa mifugo na utekaji nyara wa watoto.

    Maneja programu wa Shirika la kikristo la kuhimiza Amani na Maendeleo Bw. Lual John amesema kwenye mazungumzo hayo ya siku mbili kuwa vijana kutoka majimbo ya Boma na Jonglei, wamedhamiria kukomesha migogoro ya kikabila, pamoja na utekaji nyara wa watoto na wizi wa mifugo.

    Amesema mazungumzo hayo yanalenga kupuuza kulipiza kisasi na kuhimiza makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwezi Mei kati ya makabila hasimu chini ya usuluhishi wa makamu wa kwanza wa rais wa nchi hiyo Bw. Taban Deng Gai, na Tume ya Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako