• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria yasema kundi la Boko Haram limeanza kutumia droni na mamluki dhidi ya jeshi

    (GMT+08:00) 2018-11-30 09:14:28

    Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa kundi la kigaidi la Boko Haram sasa limeanza kutumia teknolojia ya hali ya juu kufanya mashambulizi dhidi ya jeshi la Nigeria katika sehemu ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

    Taarifa iliyotolewa na mkuu wa jeshi Jenerali Tukur Buratai amesema katika miezi miwili au mitatu iliyopita, wameshuhudia ongezeko la matumizi ya ndege zisizo na rubani dhidi ya jeshi la Nigeria na kuingia kwa wapiganaji wageni.

    Amesema kati ya Novemba 1 na 18 kundi hilo limefanya mashambulizi matano dhidi ya jeshi, lakini mashambulizi hayo yalizuiwa. Umoja wa mataifa umesema kundi hilo linaleta changamoto kubwa ya usalama, hali ya kibinadamu na utawala. Mpaka sasa kundi hilo limekuwa na operesheni nchini Cameroon, Chad, Niger na Nigeria, na mpaka sasa limefanya watu zaidi ya milioni 2.4 kwenye eneo za Ziwa Chad wakimbie makazi yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako