• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Mnangagwa ataka kuwepo kwa uwazi kwenye uteuzi wa wajumbe wa bodi kwenye mashirika ya umma

    (GMT+08:00) 2018-11-30 09:14:51

    Ikulu ya Zimbabwe imesema inawaalika watu wenye ujuzi kuomba nafasi mbalimbali kwenye bodi za mashirika mbalimbali ya umma, ili kuhakikisha uwazi kwenye uteuzi wa wajumbe wa bodi na kuimarisha ufanisi.

    Hatua hiyo inafuatia kupitishwa kwa sheria ya mashirika ya umma, inayotaka kitengo cha mashirika hayo kwenye ofisi ya Rais na baraza la mawaziri, kuwa na orodha ya majina ya watu wanaofaa kuwa wajumbe wa bodi za mashirika ya umma.

    Taarifa iliyotolewa na kitengo hicho inasema bodi za mashirika ya umma zinatakiwa kuwaalika watu mbalimbali wenye ujuzi, uzoefu, elimu na sifa za kitaaluma kuwasilisha taarifa zao, kwenye maeneo wanayoona kuwa wanaweza kuwa na ufanisi wa kiutendaji.

    Wakati hayo yanaendelea chama kikubwa cha upinzani nchini Zimbabwe MDC kimefanya maandamano ya pili kulalamikia hali mbaya ya kiuchumi, na kutoa mwito wa kuwepo kwa mazungumzo ya kisiasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako