• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamati ya uchumi wa Afrika ya UM yapongeza matokeo ya kongamano kuhusu miundo mbinu

    (GMT+08:00) 2018-11-30 09:15:11

    Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa imesema matokeo makubwa ya kongamano lililoisha hivi karibuni kuhusu maendeleo ya miundo mbinu barani Afrika, limetia msukumo mpya kwenye utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu itakayoleta mabadiliko makubwa barani Afrika.

    Kwenye kongamano hilo lililofanyika mjini Victoria Falls, mwito umetolewa wa kuendeleza miundo mbinu ya kuvuka mipaka ili kuharakisha mafungamano ya kiuchumi na kijamii, kwa maendeleo ya watu wake.

    Taarifa iliyotolewa na kamati hiyo imesema miundo mbinu hasa ili ya kuvuka mipaka ya nchi, itaimarisha mafungamano ya kikanda, na ni msingi mzuri wa nguvu ya kuimarisha ongezeko la uchumi barani Afrika. Wataalamu na watunga sera wametoa mwito kwa nchi za Afrika kuongeza miradi inayojengwa kutoka asilimia 32 za sasa hadi asilimia 50, ili kufikia malengo ya maendeleo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako