• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatarajia mkutano wa kilele wa G20 utapata mafanikio

  (GMT+08:00) 2018-11-30 09:36:17

  Mkutano wa kilele wa 13 wa kundi la nchi 20 (G20) utafanyika nchini Argentina. Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng jana alipozungumzia matarajio kuhusu mkutano huo alisema, hivi sasa hatari na changamoto zinazoukabili uchumi wa dunia zinaongezeka, hasa sera ya kujilinda kibiashara na siasa ya upande mmoja zinaathiri vibaya ongezeko la uchumi wa dunia, na pande mbalimbali zinatakiwa kushirikiana na kukabiliana na hali hiyo kwa pamoja.

  Amesema China inapenda kushirikiana na pande nyingine kuimarisha ushirikiano kwenye biashara na uwekezaji, kufungua mlango zaidi na kutafuta msukumo mpya wa ongezeko la uchumi.

  Habari nyingine zinasema, mchumi mmoja wa Afrika Kusini alimtaka rais Cyril Ramaphosa atumie fursa ya mkutano wa kilele wa G20, kuvutia biashara na uwekezaji mpya.

  Profesa Jannie Rossouw ambaye ni mkuu wa chuo cha uchumi na biashara cha Chuo kikuu cha Wits amesema, rais Ramaphosa anatakiwa kuvutia uwekezaji Afrika Kusini, na kufahamisha kuwa nchi hiyo ni salama kwa uwekezaji. Vilevile rais anatakiwa kuthibitisha utulivu wa sera ili kuhakikisha nchi hiyo inavutia uwekezaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako