Benki ya Dunia imetangaza kuwekeza dola za kimarekani milioni 45 katika kusimamia kwa ufanisi maeneo ya hifadhi nchini Msumbiji ili kuyafanya yavutie uwekezaji, na kuboresha maisha ya watu wanaoishi katika maeneo hayo. Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini Msumbiji Bw. Mark Lundell amesema usimamizi endelevu wa raslimali ni muhimu katika kupunguza umaskini na kuhimiza ustawi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |