• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yaahidi kuendeleza elimu kwa watoto ili kupunguza umasikini

  (GMT+08:00) 2018-11-30 19:19:14

  Makala iliyotolewa na wizara ya elimu ya China imesema, China imeahidi kuendelea na juhudi za kuboresha elimu kwa watoto katika maeneo yenye umasikini uliokithiri.

  Makala hiyo imeandikwa na waziri wa elimu wa China Chen Baosheng na kuchapishwa kwenye gazeti la kila siku la Guangming. Katika Makala hiyo, Chen ametoa wito kwa juhudi zaidi ili kuleta uwiano wa rasilimali za elimu kati ya maeneo ya mijini na vijijini. Amesema China imechukua hatua kadhaa katika kutekeleza hilo, ikiwemo kuboresha vifaa katika shule na lishe bora kwa wanafunzi, pia kusaidia wanafunzi zaidi kutoka vijijini na maeneo yenye hali duni kiuchumi kupata fursa ya elimu ya juu.

  Pia waziri huyo amesema, serikali kuu ya China imetumia dola za kimarekani bilioni 23 katika kuboresha vifaa na ukarabati wa karibu shule zaidi ya laki 2 za vijijini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako