• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Latin Amerika wapata matokeo makubwa

  (GMT+08:00) 2018-11-30 19:23:52

  Ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na nchi za Latin Amerika na Caribbean umepata matokeo makubwa katika miaka ya hivi kabiruni, huku pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" likileta fursa mpya kwa maendeleo zaidi ya ushirikiano huo kati ya pande hizo mbili.

  Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka jana thamani ya biashara kati ya China na nchi za Latin Amerika na Caribbean ilifikia dola za kimarekani bilioni 257.8, ambayo ni ongezeko la asilimia 18.8 kuliko mwaka 2016. Katika miezi tisa ya mwanzo ya mwaka huu, thamani ya biashara hiyo imeongezeka kwa asilimia 20 na kufikia dola za kimarekani bilioni 228.6.

  Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng amesema, uchumi wa China na nchi za Latin Amerika unanufaishana, uwezo wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili ni mkubwa, na China ina imani kwa mustakabali wa ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako