• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNICEF yasema udhibiti wa maambukizi ya UKIMWI kwa vijana bado hauridhishi

    (GMT+08:00) 2018-11-30 19:26:37

    Ripoti iliyotolewa na Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF imeonesha kwamba, huenda vijana laki 3.6 watafariki itakapofika mwaka 2030 kutokana na magonjwa nyemelezi yanayosababishwa na UKIMWI kama nguvu zaidi hazitaongezwa katika kuzuia, kugundua na kutibu ugonjwa huo.

    Ripoti hiyo imesema, hivi sasa, vijana milioni 3 wanaishi na virusi vya HIV. Mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Henrietta Fore amesema, ingawa wamepata mafaniko katika kuzuia kueneo kwa virusi hivyo kutoka kwa mama kwenda kwa watoto, lakini udhibiti wa kuenea kwa virusi hivyo kwa vijana bado haujafikia kiwango kilichopangwa.

    Ripoti hiyo imeshauri kwamba, ni bora kutumia jukwa la kidijitali kutoa elimu kwa vijana kuhusu ugonjwa huo na kutoa huduma inayoendana na tabia za vijana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako