• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaunga mkono shughuli za haki za wapalestina

    (GMT+08:00) 2018-11-30 19:34:09

    Balozi wa kudumu wa China kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Vienna Bw. Wang Qun amesema China inafuatilia sana suala la Palestina, na inaunga mkono shughuli za haki za kurudisha haki halali za kikabila kwa wapalestina.

    Bw. Wang Qun amesema hayo katika hafla ya Siku ya Kimataifa ya Kuunga mkono Wapalestina iliyofanyika jana. Amesema katika mkutano wa ngazi ya mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na nchi za Kiarabu uliofanyika mwezi Julai mwaka huu, China ilitangaza tena kutoa misaada ya dharura ya kibinadamu na kuongeza kutoa fedha kwa idara ya kuwasaidia wakimbizi wa Palestina ya Umoja wa Mataifa.Amesema China inapenda kuendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa, kurekebisha njia ya kimataifa ya kuhimiza amani, kuhamasisha Palestina na Israel kuanzisha tena mazungumzo ya amani, na kufanya juhudi kwa kutimiza amani ya pande zote, haki na utulivu wa Mashariki ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako