• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China atoa makala kwenye gazeti la La Estrella la Panama

  (GMT+08:00) 2018-11-30 21:10:10

  Rais Xi Jinping wa China ametoa makala yenye kichwa cha "Shirikiana kujenga mustakabali mzuri" kwenye gazeti la La Estrella la Panama, kabla ya kuanza ziara rasmi nchini humo.

  Kwenye makala hiyo, rais Xi amesema, mawasiliano ya kirafiki kati ya watu wa China na Panama yameendelea kwa zaidi ya miaka 160, na mwezi Juni mwaka jana, China na Panama ziliamua kuanzisha uhusiano wa kibalozi. Tangu wakati huo, ushirikiano katika sekta mbalimbali kati ya nchi hizo mbili umekua na kuleta manufaa halisi kwa wananchi wao.

  Kwa sasa Panama inatekeleza mkakati wa mwaka 2030 wa usambazaji wa bidhaa, na inajitahidi kujenga kituo cha usambazaji wa bidhaa chenye kiwango cha kimataifa, mkakati huo unalinganishwa na pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja". China inapenda kushirikiana na Panama kufanya juhudi ili kuimarisha muungano wa mikakati ya maendeleo ya nchi hizo mbili, na kunufaisha zaidi watu wao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako