Mkutano wa kilele wa 13 wa kundi la nchi 20 (G20) ulifanyika jana huko Buenos Aires nchini Argentina, ambapo Rais Xi Jinping ametoa hotuba muhimu na kutoa mapendekezo manne.
Akitaja mapendekezo hayo rais Xi Jinping amelitaka kundi la nchi 20 lishikilie ushirikiano na kufungua mlango, na kulinda utaratibu wa biashara unaoshirikisha pande nyingi. Na pia amezitaka pande mbalimbali zishikilie moyo wa wenzi, na kuimarisha uratibu wa sera. Aidha Rais Xi pia amelitaka kundi la G20 lishikilie uvumbuzi na kutafuta nguvu mpya ya kuhimiza ongezeko la uchumi. Vilevile amelitaka kundi hilo lishikilie maendeleo ya pamoja, na kuhimiza maendeleo yanayonufaisha nchi nyingi, hasa kulinda maslahi ya nchi zinazoendelea.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |