• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Russia wafanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2018-12-01 16:02:15

    Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia Vladimir Putin jana walikutana huko Buenos Aires.

    Rais Xi amesema, kuanzia mwaka huu China na Russia zimefanya jitihada kwa pamoja na kupata mafanikio mfululizo kwenye ushirikiano wa sekta mbalimbali.

    Rais Xi amezitaka China na Russia ziendelee kuunganisha ujenzi wa Ukanda Mmoja na Njia Moja na Muungano wa uchumi wa Ulaya na Asia, na kuzidisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika mambo ya uchumi na biashara, fedha, nishati na teknolojia.

    Kwa upande wake rais Putin amesema Russia itashirikiana na China kuimarisha ushirikiano kwenye sekta mbalimbali, na kutoa mchango katika kulinda Amani na usalama wa dunia, na kujenga uchumi wa dunia ulio wazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako