• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe asema kauli za kukosoa misaada ya China kwa Afrika si sahihi

    (GMT+08:00) 2018-12-01 16:38:25

    Hafla ya kuweka jiwe la msingi kwenyeujenzi wa bunge la Zimbabwe linalojengwa na China, imefanyika Harare, Zimbabwe. Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ametoa hotuba kwenye hafla hiyo na kuishukuru China kwa msaada wake wa moyo wa dhati na kudhihirisha kuwa kauli za kukosoa misaada ya China kwa Afrika si sahihi.

    "Watu na nchi kadhaa wanakosoa misaada ya China kwa Afrika, lakini kauli hizo si sahihi. Nilipofanya ziara nchini China mwaka huu, baadhi ya watu waliniambia kuwa hawaendi China, lakini nilikutana nao wakitafuta fedha kutoka China, pia niliwaona watu kutoka Magharibi wakitafuta fedha Beijing. "

    Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Makamu wa rais wa Zimbawe Bw. Constantino Chiwenga, na Bw. Kembo Mohadi, mawaziri, wabunge wote, maafisi wakuu wa serikali, mabalozi wa nchi mbalimbali nchini Zimbabwe na wawakilishi wa kampuni za China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako