• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa BRICS wakubaliana kushikilia mfumo wa pande nyingi

    (GMT+08:00) 2018-12-01 16:41:07

    Viongozi wa nchi zinazoibukia kiuchumi BRICS jana walifikia makubaliano kadhaa pembeni mwa mkutano wa kundi la nchi 20, juu ya kushikilia mfumo wa pande nyingi na sheria zinazofuata utaratibu wa dunia.

    Katika mkutano huo usio rasmi ulioongozwa na rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ambaye ni mwenyekiti wa zamu, viongozi pia walibadilishana mawazo kwa kina juu ya uchumi wa dunia, changamoto zilizopo na ushirikiano ndani ya BRICS. Akiongea kwenye mkutano huo Rais wa China Xi Jinping amesema viongozi wa BRICS walikuwa na mkutano uliozaa matunda mwezi Julai mwaka huu huko Johannesburg, ambapo walifikia makubaliano muhimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako