Rais Xi alitoa kauli hiyo katika chakula cha jioni pamoja na rais Trump, akiongeza kuwa anafurahia kukutana na rais Trump.
Baada ya makutano yaliyopita, rais Xi alisema, hali ya dunia imebadilika sana. China na Marekani zikiwa ni nchi mbili zenye nguvu kubwa za ushawishi zinapaswa kubeba wajibu muhimu katika kuimarisha amani na ustawi duniani, huku ushirikiano ndio ni njia nzuri zaidi.
Marais hao walikubaliana mwezi uliopita walipoongea kwa simu kwamba wangekutana katika kipindi cha mkutano wa kilele wa kundi la G20, ambapo rais Xi alisema yeye na rais Trump wote wana imani na ushusiano wa China na Marekani pamoja na uhusiano wa kiuchumi na kibiashara.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |