• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi na Trump wakubaliana kuacha kuongeza ushuru wa forodha

    (GMT+08:00) 2018-12-02 11:44:41

    Marais wa China na Marekani wamekubaliana kuacha hatua za kutozana ushuru nyongeza wa forodha.

    Hayo yametangazwa na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi baada ya mazungumzo kufanyika kati ya rais Xi Jinping na rais Donald Trump Jumamosi jioni huko Buenos Aires, Argentina.

    Marais hao walijadili masuala ya uchumi na biashara, na kufikia makubaliano muhimu, huku wakitoa mapendekezo kadha wa kadha kuhusu namna ya kuondoa tofauti na kutatua masuala yaliyopo. Kwa upande wa China, katika juhudi za kuleta uwiano wa kibiashara, inapenda kuagiza bidhaa za Marekani kulingana na mahitaji ya soko na wateja wa China. Marais hao wamekubaliana kila nchi kufungua soko lake kwa nchi nyingine, na matakwa yenye haki ya Marekani yatazingatiwa katika mchakato wa China kuendeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango. Maofisa wa nchi mbili watafanya mazungumzo haraka kwa msingi wa makubaliano yaliyofikiwa na marais wao, ili kufikia makubaliano halisi mapema kwa lengo la kuondoa kabisa ushuru wa nyongeza wa forodha.

    Rais Xi Jinping na rais Donald Trump walikula chakula cha jioni pamoja na kufanya mazungumzo kwa saa mbili na nusu Jumamosi jioni, huko Buenos Aires. Mkutano uliopita kati ya marais hao ulifanyika mwezi Novemba mwaka jana hapa Beijing.

    Habari zinasema pande zote mbili zinaona makubaliano ya kikanuni yaliyofikiwa katika mazungumzo hayo yana maana kubwa, kwamba yanazuia mikwaruzano ya kibiashara isizidi kuwa mibaya, na kuleta matumaini mapya ya ushirikiano wa kunufaishana, hali ambayo si kama tu inasaidia maendeleo ya China na Marekani na kulingana na manufaa ya watu wao, bali pia inachangia ongezeko la uchumi wa dunia na manufaa ya nchi mbalimbali.

    Kwenye mazungumzo hayo, marais hao pia walijadili masuala mengine yakiwemo kuimarisha ushirikiano katika kupambana na dawa za kulevya, na hali ya peninsula ya Korea. China imerudia msimamo wake wa kikanuni kuhusu suala la Taiwan, na Marekani imesisitiza kushikilia sera ya kuwepo kwa China moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako