• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Raia 206 wauawa kwenye mashambulizi ya ndege nchini Syria katika mwezi Novemba

    (GMT+08:00) 2018-12-02 16:48:51

    Watu 206 waliuawa katika mwezi Novemba kwenye mashambulizi ya ndege yaliyofanywa na muungano unaoongozwa na Marekani kwenye maeneo yanayodhibitiwa na kundi la IS, mashariki mwa Syria.

    Shirika la kufuatilia haki za binadamu nchini Syria, limesema watoto 77 na wanawake 57 ni kati ya watu waliouawa kwenye ngome ya mwisho ya kundi la IS katika maeneo ya vijijini ya Jimbo la Deir al-Zour.

    Muungano wa majeshi yanayoongozwa na Marekani uliongeza mashambulizi yake katika wiki za hivi karibuni kuwaunga mkono wapiganaji wa kundi la wakurd la SDF, linalojaribu kuwaondoa wapiganaji wa kundi la IS kutoka kwenye ngome yao, ukingo wa mashariki wa mto Euphrates. Hata hivyo mashambulizi ya kujibu yanayofanywa na wapiganaji wa kundi la IS yamekwamisha juhudi za kundi la SDF.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako