• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran imesema itaendelea kutengeneza na kufanya majaribio ya makombora bila kujali upinzani wa Marekani

    (GMT+08:00) 2018-12-03 08:35:14

    Iran imesema itaendelea kutengeneza na kufanya majaribio ya makombora kwa ajili ya ulinzi wake, licha ya msimamo wa kupinga wa maofisa wa Marekani.

    Msemaji wa jeshi la Iran Bw. Abolfazl Shekarachi amesema majaribio ya makombora na uwezo wa jumla wa kujilinda wa Iran, ni kwa ajili ya ulinzi na sera yake ya kukabiliana na matishio. Amesema Iran itaendelea na majaribio ya makombora, na suala hilo liko nje ya majadiliano yoyote na ni sehemu ya usalama wa taifa.

    Bw. Shekarachi amesema hayo kufuatia kauli ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo aliyesema majaribio ya makombora ya Iran yanakwenda kinyume na azimio nambari 2231 la Baraza la usalama la Umoja wa mataifa. Bw. Pompeo alisema hayo baada ya Iran kufanya majaribio ya kombora la masafa ya kati linalobeba vichwa kadhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako