• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa UM azihimiza nchi za Afrika kukopa kwa sarafu zao ili kuboresha uwezo wao wa kuhimili madeni

    (GMT+08:00) 2018-12-03 08:38:08

    Ofisa wa Umoja wa mataifa amezihimiza nchi za Afrika kukopa kwa sarafu zao ili kuboresha uwezo wao wa kuhimili madeni. Katibu mtendaji wa Kamisheni ya kiuchumi ya Umoja wa mataifa kwa Afrika Bibi Vera Songwe amesema mjini Nairobi kuwa bara la Afrika litahitaji kushirikiana na soko la fedha na wakopeshaji wa mikopo nafuu kama vile Benki ya dunia na Benki ya maendeleo ya Afrika, ili kusaidia kupunguza hatari ya kukopa kwa sarafu za kiafrika.

    Amesema madeni ya sarafu za kiafrika yaliyotolewa katika nchi zao au nchi za nje yanaweza kuisaidia Afrika kupunguza hatari inayotokana na kiwango cha ubadilishaji wa fedha ambacho husababisha msukosuko wa madeni. Kwa mujibu wa ofisa huyo, Rwanda na Afrika Kusini zimetoa madeni kwa sarafu zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako