• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkuu wa UNAMID athibitisha kuboreka kwa usalama huko Darfur

    (GMT+08:00) 2018-12-03 08:38:31

    Mwakilishi maalumu wa pamoja wa Tume ya Umoja wa mataifa katika eneo la Darfur Bw. Jeremiah Mamabolo amethibitisha kuboreka kwa hali ya usalama huko Darfur, lakini pia ameonya dhidi ya kuongezeka kwa wakimbizi wa ndani kwenye kanda hiyo.

    Amesema watu waliokimbia makazi yao wameanza kurudi nyumbani baada ya hali ya usalama kuboreka kwenye sehemu nyingi za Darfur, lakini kanda hiyo bado inashuhudia mawimbi mapya ya wakimbizi wa ndani, haswa kwenye eneo la Jebel Marra, ambako mapambano kati ya makundi yenye silaha na vikosi vya serikali yameendelea kuwaathiri wakazi wa eneo hilo.

    Bw. Mamabolo ametoa wito kwa makundi hayo kujiunga na mchakato wa amani ili kutimiza amani ya kudumu kwenye kanda ya Darfur. Pia ameongeza kuwa tume ya UNAMID inaendelea na mpango wake wa kuondoka Darfur hatua kwa hatua, kwa mujibu wa azimio namba 2429 la Baraza la usalama la Umoja wa mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako