• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Argentina zahimiza maendeleo ya uhusiano mpya kati yao

    (GMT+08:00) 2018-12-03 08:52:34

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na kufanya mazungumzo na mwenzake wa Argentina Mauricio Macri na kukubaliana kuhimiza maendeleo ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi zao.

    Rais Xi amesema, pande hizo mbili zinatakiwa kuungana mkono katika masuala yanayohusiana na maslahi makuu ya kila upande na chaguo lao la njia ya kujiendeleza. Pia amesema mwaka huu China imechukua hatua katika kuisaidia Argentina kudumisha utulivu wa kifedha. Amependekeza pande hizo mbili ziongeze ushirikiano na mawasiliano ndani ya mfumo wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na kuratibu mipango yao ya maendeleo.

    Bw. Macri ameishukuru China kwa misaada yake ya muda mrefu na kuipongeza China kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya miaka 40 tangu ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango. Pia amesema maendeleo ya China yana maana kubwa kwa maendeleo ya Argentina na Latin Amerika na amani na utulivu na ustawi wa dunia. Katika ziara hiyo rais Macri amemtunuku rais Xi Jinping tuzo ya juu ya Argentina ya mkombozi San Martin.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako