• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Comey afikia makubaliano na wabunge wa Republican kuhusu ushahidi wake

    (GMT+08:00) 2018-12-03 09:25:23

    Aliyekuwa mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la Marekani FBI Bw. James Comey amesema amefikia makubaliano na wabunge wa chama cha Republican juu ya ushahidi wake kuhusu hatua zilizochukuliwa na FBI kabla ya uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka 2016. Amesema anapenda kushiriki kwenye mkutano wa kusikiliza kesi ulio wazi. Wanachama wa Republican wanataka kumhoji Bw. Comey kuhusiana na uchunguzi wake dhidi ya Bibi Hillary Clinton kwa kutumia barua pepe binafsi wakati alipokuwa waziri wa mambo ya nje na tuhuma za kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako