• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi aanza ziara ya kitaifa nchini Panama

    (GMT+08:00) 2018-12-03 10:49:40

    Rais Xi Jinping wa China amewasili Panama City na kuanza ziara ya kitaifa nchini Jamhuri ya Panama. Rais Juan Carlos Varela na mkewe Bibi Lorena Castillo GarcĂ­a de Varela waliwalaki rais Xi na mkewe Bibi Peng Liyuan katika uwanja wa ndege na kuwaandalia dhifa ya kuwakaribisha.

    Rais Xi amesema hii ni mara ya kwanza kwake na kwa rais wa Jamhuri ya Watu wa China kufanya ziara nchini Panama. Amesema, mwaka mmoja na nusu uliopita, China na Panama zilianzisha uhusiano wa kibalozi katika msingi wa kanuni ya kuwepo kwa China moja, na kufungua ukurasa mpya kwa historia ya mawasiliano ya miaka 160, jambo ambalo linalingana na maslahi ya kimsingi na muda mrefu ya nchi hizo mbili na wananchi wake, na ushirikiano kati ya pande hizo mbili unaweza kuendelezwa zaidi.

    Ameongeza kuwa anatarajia kupanga mpango wa maendeleo ya muda mrefu ya uhusiano kati ya China na Panama, kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana, kuhimiza maendeleo ya pamoja na kuzinufaisha nchi hizo mbili na wananchi wake.

    Panama ni kituo cha tatu katika ziara yake, na baadaye anatarajiwa kufanya ziara nchini Ureno.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako