• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji 80 wa kundi la Taliban wauawa kaskazini na mashariki mwa Afghanistan

    (GMT+08:00) 2018-12-03 15:46:41

    Wapiganaji 80 wa kundi la Taliban wameuawa katika operesheni iliyofanywa na vikosi vya usalama vya Afghanistan katika mkoa wa Balkh ulioko kaskazini na mkoa wa Ghanzi ulioko mashariki mwa nchi hiyo.

    Msemaji wa serikali ya mkoa wa Balkh Bw. Munir Ahmad Farhad amesema, wapiganaji 50 wa kundi la Taliban wameuawa na wengine zaidi ya 70 wamejeruhiwa katika wilaya za Chamtal, Charbolak na Dawlat Abad mkoani humo. Amesema mahandaki na silaha kadhaa za wapiganaji hao pia ziliharibiwa katika mapigano kati ya kundi hilo na jeshi la serikali.

    Wakati huohuo, taarifa iliyotolewa na jeshi la Afghanistan imesema, wapiganaji 30 wa kundi la Taliban wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika operesheni inayoendelea kwenye eneo la Rasana lililoko wilaya ya Jaghori, mkoa wa Ghazni nchini humo. Taarifa hiyo imesema, operesheni hiyo ilianza jana, na mpaka sasa, vikosi vya usalama vya nchi hiyo vimefanikiwa kudhibiti tena vijiji kadhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako