• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakuu wa majeshi ya Uganda na DRC wakubaliana kufanya doria ya pamoja kwenye eneo la mpaka

    (GMT+08:00) 2018-12-03 16:41:45

    Wakuu wa majeshi ya Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamekubaliana kufanya doria ya pamoja katika eneo la mpaka katika Ziwa Albert na Ziwa Edward, ambalo hivi karibuni lilikumbwa na mashambulizi, utekaji nyara, na mauaji.

    Msemaji wa jeshi la Uganda Brigedia Richard Karemire amesema, pande hizo mbili zimekubaliana kufanya ushirikiano na uratibu kati ya makamanda wa majeshi ya nchi hizo mbili, kama njia ya kudhibiti na kupunguza matukio yanayoharibu usalama katika eneo hilo. Ameongeza kuwa pande hizo mbili zimekubaliana kuendelea kubadilishana taarifa za kipelelezi, kukutana, na kufanya doria ya pamoja ili kuondoa wasiwasi wa usalama katika maziwa hayo, na kuhakikisha usalama na amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako