• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya mambo ya nje ya China yasema mkutano wa kilele wa G20 umepata mafanikio mengi

    (GMT+08:00) 2018-12-03 19:23:53

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, mkutano wa kilele wa kundi la nchi 20 (G20) uliomalizika hivi karibuni umepata mafanikio makubwa.

    Amesema, China ina imani kuwa kama nchi wanachama wa G20 zikiendelea kushikilia msimamo wa utawala wa dunia wenye majadiliano, ujenzi na ushirikiano wa pamoja, kubeba wajibu wa jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja na kuimarisha ushirikiano na mshikamano, zitaweza kutoa mchango mkubwa katika kuhimiza maendeleo ya uchumi wa dunia na kuzidi kuwanufaisha watu wa nchi mbalimbali.

    Mbali na hayo, Bw. Geng amesema, China imemaliza zamu yake ya kuwa nchi mwenyekiti wa zamu wa mwezi wa Novemba wa Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa, na kazi iliyofanywa na China imepongezwa na pande mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako