• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa apongeza wakuu wa G20 kufikia makubaliano mbalimbali

    (GMT+08:00) 2018-12-03 19:50:33

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amepongeza makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa kwenye mkutano wa 13 wa wakuu wa kundi la G20, ikiwemo suala la maendeleo endelevu na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Bw. Guterres amesema, azimio la mkutano wa kilele wa Buenos Aires la wakuu wa G20 limedhihirisha kuwa viongozi hao wamegundua umuhimu wa kutatua suala la biashara kwa kupitia njia ya pande nyingi, na mageuzi ya Shirika la Biashara Duniani (WTO), na kusisitiza tena kujitahidi kutimiza ahadi ya kufuata utaratibu wa kimataifa unaozingatia sheria. Aidha Azimio hilo limethibitisha uungaji mkono wake kwa Agenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu. Pia katibu mkuu huyo ameeleza kuunga mkono ahadi zilizotolewa na wakuu wa G20 kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako