• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Serikali ya Tanzania haiwezi kukata ushuru kwa bei ya 3,000 ya korosho

    (GMT+08:00) 2018-12-03 20:12:07

    Uamuzi wa Serikali kuingilia mauzo ya korosho kwa kupanga bei ya Sh3,300 kwa kilo bila kuwa na makato yoyote, umepokelewa kwa furaha kubwa na wakulima ambao wameuona kuwa huo ni uamuzi mzuri na neema kwao.

    Hata hivyo yapo mambo yanayohitaji kufanyiwa kazi kwa faida ya siku zijazo kwa wakulima, maendeleo ya zao hilo na jamii kwa ujumla.

    Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Newala, Mussa Simaye alisema kwa sasa wanasubiri tamko la Serikali kwani kwa bei ya Sh3,300 hawatarajii kupata ushuru wa korosho.

    Simaye alisema mapato hayo hupatikana kutokana na mjengeko wa bei ambapo halmashauri hupata asilimia 3 katika bei elekezi ambayo mwaka jana ilikuwa Sh1,400.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako